Young Killer arekodi wimbo na Fid Q , aupa jina la tarehe yao ya kuzaliwa ’13’, umefanywa na maproducer 4 akiwemo Majani


Rapper kutoka Rock City, Young killer Msodoki wiki hii amerekodi wimbo mpya ambao amemshirikisha kaka yake rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, ambaye pia anatoka Mwanza. Msodoki amezungumza kuhusu wimbo huo, “Ni project mpya kabisa kali naweza kusema kwasababu imekutanisha wakali wawili halafu kutoka mji mmoja”,  Killer. Amesema kuwa jina la wimbo ni tarehe yao ya kuzaliwa ’13’