Msemaji wa Jumuia ya nchi za Pembe ya Afrika, (IGAD) alieleza kuwa baada ya mazungumzo ya siku mbili mjini Addis Ababa, pande zinazopigana Sudan Kusini zimekubali kusitisha vita moja-kwa-moja.
Pande hizo zilionywa yatayofwata iwapo zitavunja makubaliano, kama alivotamka msemaji wa IGAD.
"Makubaliano ya kusitisha mapigano yakivunjwa na upande wowote ule, hatua zinazofuata zitachukuliwa na Jumuia ya IGAD:
Mali za pande hizo zitazuwiliwa.
Wanasiasa watapigwa marufuku kusafiri katika eneo la IGAD
Silaha na risasi zitazuwiliwa kupelekwa Sudan Kusini, pamoja na zana zote zinazoweza kutumiwa kwenye vita"

0 Comments