Ukosefu wa Vyoo nchini India


Jimbo la Gujarati nchini India linataka iwe sheria kwa mtu yeyote anayetaka kuwania wadhfa wa uma kuwa na choo nyumbani mwake,ili kuzuia watu kwenda haja katika maeneo yalio wazi.
Mswada uliopitishwa na bunge la Gujarati siku ya jumatatu pia unataka viongozi waliochaguliwa kubaini katika kipindi cha miezi sita iwapo wana vyoo nyumbani la sivyo waondolewe katika nyadhfa zao.
''Kukabiliana na watu wanaokwenda haja katika maeneo ya wazi ni muhimu kwa lengo la kuimarisha mazingira safi mbali na uchafuzi wa maji','ilisema serikali.
Gujarat ni jimbo la nyumbani la waziri mkuu mpya Narendra Modi ambaye amesema kuwa kila nyumba ni sharti imiliki choo katika kipindi cha miaka minne ili kuzuia magonjwa yanayosababishwa na watu kwenda haja katika maeneo ya wazi.
Hatari zinazowakumba wanawake wanaokwenda haja nchini India
Mamilioni ya raia nchini India hawana vyoo.
Hatahivyo raia hao wanadaiwa kuwa na tatizo la utumizi wa vyoo.hii ni kwa sababu kila sekunde mtu mmoja huenda haja katika eneo la wazi,swala linalosababisha ugonjwa wa utapia mlo miongoni mwa watoto, kushuka kwa uchumi pamoja na ghasia dhidi ya wanawake.
Ni tatizo ambalo waziri mkuu Narendra Modi ameamua kuhakikisha kuwa kila nyumba ina choo ifikiapo mwaka 2019.
Lakini kulingana na wataalam wa usafi ,jibu halitapatikana iwapo kutajengwa vyoo zaidi vya kuogea ,kwanza raia ni sharti waanze kupendelea kwenda katika vyoo.