Raia wa ufaransa wakipinga mauaji ya Charlie Hebdo
Zaidi ya watu milioni moja wanatarajiwa kushiriki kwenye matembezi katika mji mkuu wa ufaransa hii leo kupinga mauaji ya watu 17 yaliyofanywa na wanamgambo wa kiislamu.
Karibia viongozi 40 wa nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria matembezi hayo akiwemo rais wa Palestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Maelfu ya polisi na wanajeshi wako eneo hilo huku ulinzi mkali ukiwekwa.
Ghasia zilianza siku ya jumatano wakati watu waliokuwa na silaha walipowapiga risasi wafanyakazi wa gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo ambapo watu 12 waliuwa.
Siku ya Ijumaa naye mwanamume mmoja aliwaua watu wanne kwenye duka moja la jumla.